Mapenzi Lyrics

von Kidum
Lyrics
Ooooo yeyeee
Mapenzi ooohh
Kama ni mapenzi
Ya kuniudhi kila saa
Ya kunifanya mi kulia
Na kama huridhiki
Na mbona hujasema
Ili niweze rekebisha
Ilifaa ni mambo shwari
Nikiamini u kwangu

Na kukusifu kwa wazazi
Hujali tena hisia zangu

Sijui tunapokwenda
Lakini najua tulipotoka
Kutoka sitoki nimetekwa nyara
Kukuwacha siwezi kibarua ngumu
Nashindwa ni nini ntafanya uridhike
Nimetekwa ndani

Mtandao wa mapenzi

Basi nakuomba
Uniteke tu bila mateso
Tazama, nimezama
Ndani ya bahari
La penzi lako
Siwezi
Kusonga mbele
Kurudi nyuma

Sijielewi
Haya mapenzi ya fujo hayafai

Kama wanipenda
Jaribu kunipa raha
Mi nashangaa
Watu wakisema
Eti tunapendana
Japo tunazozana
Ni vizuri mami
Nyumba kuwa na siri
Lakini jaribu
Tusuluhishe
Bila hivyo
Itakuwa mchezo
Wa kuigiza

Kwenye mambo bandia
Mimi sitaki
Mambo ya kujifanya

Ati tunapendana
Tena tunatesana
Nimejaribu sana kujitoa ndani

Kila nikipanga napangua mwenyewe
Natamani sana ungeelewa hivyo
Mimi mateka
Mimi pumbavu

Wa penzi lako
Nieleze ni lini ntakuwa huru
Tazama, nimezama
Ndani ya bahari
La penzi lako

Siwezi
Kusonga mbele
Kurudi nyuma
Sijielewi
Haya mapenzi ya fujo hayafai
Kama wanipenda
Jaribu kunipa raha
Jaribu baby
Mambo
Ya kunifanya kumbafu haifai
Mambo yo yo yo yo yo
Haifai
Jaribu baby
Tusuluhishe
Writer(s): Nimbona ''kidum'' Jean-pierre
Lyrics powered by www.musixmatch.com
Was als nächstes?

Dein Karma steigt mit jedem Klick! Teile den Guru-Link und bring Lyrics in die Welt.

Kidum - Mapenzi
Quelle: Youtube
0:00
0:00