[Chorus]
Hey! Baby,
Nataka kukuona,
Sura yako inafanya roho inapona.
Eei! Kweli we ni malaika,
Hao wengine nawaita kadhalika.
[Verse 1]
Kaa kuna mtu hii dunia ana bahati ni mimi,
Najua kila mtu ataniuliza kwa nini,
Manzi yangu bumba hata mi siamini,
Sitaki Ruth, sitaki Ray, sitaki pia Kanini.
Kushikwa nimeshikwa nikawekwa mfuko,
Hakuna pickpocket atanitoa huko,
Ni mimi na yeye,
Yeye na mimi,
Tuko pamoja kama mdomo ulimi.
Amekua na mimi nikikaranga chumvi,
Atakuwa na mimi nikianza kunona,
Sijamuona leo lakini story ni hii,
Nitachukua simu yangu nimuambie hivi.
Ntasema.
[Chorus]
[Verse 2]
Si kila siku utapata msichana mzuri,
Msichana amesoma ‘kini hana kiburi,
Msichana saa zingine anasoma zaburi,
Kusikiza santuri kwake pia desturi.
Kama niko na yeye kila kitu ni shwari,
Naona poa sana ananijali hali,
Ye ni upepo wangu katika jua kali,
Tafadhali please nitasema ukweli.
Akiniacha leo sitafuti mwingine,
Mambo ya kutafuta niliacha zamani,
Lakini hiyo haitafanyika jamani,
Juu hata yeye najua anafikiri hivi…
[Chorus]
[Bridge]
I have eyes for only you, for only you [x3].
[Chorus]
[end]
Lyrics powered by www.musixmatch.com